Tuesday, September 12, 2017

WIVU NI NINI


Wivu ni hisia zifananazo na
chuki zimpatazo mtu hasa
aaminipo kitu/hali flani yeye
ndiye aliyestahili kuipata kuliko
aliyepata
Wivu ni tabia kama
zilivyo tabia nyngnezo kama
uchoyo, unafiki, usaliti, uongo
nk. Pia kuna aina kuu mbili za
wivu zinazojitokeza sana ktk
maisha ya kila siku

1. Wivu wa kimapenz
2. Wivu wa maendeleo.
Nitafafanua kidogo japo kwa
mifano. ili aina hizi ziweze
kueleweka

1. Wivu wa kimapenzi
Hii ni aina ya wivu, ambao
hujitokeza baina ya watu
wawili ambao wana mahusiano
ya kimapenzi, inapotokea
mmoja kati ya watu hawa
afanyapo kitu kinachoweza
fanya aonekane kwa namna
moja au nyingine na
mahusiano ya ukaribu na jinsia
nyingine. basi mwenzie huanza
kupatwa na hisia tofauti
ambazo huambatana na kero
ya maumivu fulani fulani hivi
ambayo hayaelezeki, pata picha
ktk pita pita zako unamuona
mwenza wako na rafiki yako wa
jinsia tofauti na yake
wanatembea huku wakicheka
na kufanya michezo ya hapa na
pale.

2. Wivu wa maendeleo.
aina hii inaweza kujitokeza
hasa hasa kwa marafiki ghafla
unakuta mwenzio/jilani/ndg
yako anafanikiwa anapendeza,
akisema anasikilizwa [japo
unaamini hana point],
anajenga, ana gari nzuri,
biashara yake zinakwenda poa
ila aina ya kazi mnafanya moja
na wewe unadidimia hapa sasa
ndo wivu huu huanza
kujitokeza.
Je kuna watu wasio na wivu…..!
kuwa na Wivu si dhambi na ni
karibia watu wote tuna wivu.
isipokuwa sasa Wivu ndo
humzalishia mwanadamu
dhambi hasa anaposhindwa
kuvumilia mambo yanayomsibu
katika roho yake, hapa ndio
huzaa dhambi ya chuki,
uwongo, fitina, majungu,
uchawi n.k. Lakini kwa mwenye
akili nzuri ndo hutumia muda
huo kujisahihisha kuwa wapi
nakosea, wapi nateleza katika
kufanya mambo yangu ili
nifanikiwe.
Sababu zipelekeazo mtu kuwa
na wivu…….!

1. Kutokujiamini
hii huwatokea sana watu
waliopo ktk mahusiano mtu
anaamini kuwa mwenza wake
akitoka ndio basi tena…! Eti
atakutana na wazuri zaidi yake
hivyo tayali anakuwa na
kisilani moyoni !
Sikia mpendwa uzuri wa mtu
upo machoni pa mtu ivyo kaa
ukijua kama umechaguliwa
wewe basi we ndo bora kuliko
wote sawa…., jiamini basi.

2. Usaliti
Inapotokea mmoja kati ya
wapenzi si muaminifu hata
wakisameheane wivu huwa upo
katikati, hivi hujawahi kuona
mtu na mpnz wake wakigombea
kusoma txt ktk simu.

3. Ujinga
Pia nao husabisha kitu hiki,
mwenzio anafanya bidii katika
utafutaji, anabana matumizi,
lakini wewe ubunifu na bidii
hakuna, ila bata mwanzo
mwisho na mwisho wa siku
mnataka muwe sawa za wapi
hizo !

4. Lack of job security
unaweza nipa msaada ktk
kuiweka katika kiswahili ila ili
paeleweke vyema tizama mfano
huu unafanya kazi sehemu,
anakuja mtu amekuzidi elimu,
mcheshi, mpiga kazi n.k na
akipendwa na bosi ndio basi
tena unaanza kusema muache
anajifanya mjuaji, sijui ni
nanini ! Acha uoga, jitahidi
utengeneze alama sehemu
zako, siku ukikosekana watu
wahisi wamepungukiwa kitu.

4. Ubinafsi
Hivi ushawahi kaa na mtu
ghafla akakwambia huyu kaka/
dada simpendiiiii ! Na
ukimuuliza kwanini anakujibu
basi tuu !
Chunguza vizuri mtu wa namna
hii huwa wana tatizo dogo
sana may be anachukia mtu
kupendeza, life style yake n.k
na atazalisha sababu hapo
mara utasikia hasalimii, sijui
anajidai lakini ukiangalia
hakuna anachaothirika !

5. Urithi.
Kuna watu ambao wamezaliwa
tu kwa roho mbaya yaani
hapendi kuona watu
wakifanikiwa na sababu ya
msing hana ndo alivyo tuu.

6. Umasikini
msinielewe vibaya kwamba
matajili hawana wivu la hasha,
bali wengi huingia katika
kutamani vitu vingi mda
mwingine hata asivyo na uwezo
wa kupata kwa wakati huo.

7. Negative thinking
mfano kuhusu mtu anaringa,
anajidai, au anafanya jambo
kwa maslahi binafsi wkt
dhamila mtu huyo ni tofauti na
mawazo yako.
Jinsi ya kutengeneza jamii isiyo
na wivu

1. Kuishi kwa usawa
2. Jengeni mazingira ya
kuaminiana.
3. Kufanya kazi kwa bidii.
4. Upendo na kuheshmiana.
5. Kuishi kwa kusaidiana

Gm Artst

No comments:

Post a Comment