1. Unanunua nguo bila mpangilio
kuna watu wana nguo kama duka
Kuwa na nguo chache tu huwezi
kushindana na fashion.
2. Unanunua Viatu bila mpango,
viatu pia vinameza savings zetu,
nunua pea chache zenye ubora ili
zidumu.
3. Unatoa ofa bar bila mpango.
Nenda bar kwa bajeti mahususi.
Hakuna atakae kusifia kwa kutoa
ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu
wa kamba yake. Jifunze ubepari.
4. Unatumia hela nyingi kwenye
simu ambazo sio productive.
Unaweka vifurushi vya week vya sh
7000 au 10000 ili uchati na
marafiki Fb au Whatsaap Huo ni
ujinga. Badilika.
5. Unakopa hela benki na kununua
vitu kama simu ya milioni na gari
ambazo sio productive. Unakosa
hela hata ya mafuta, gari la nini
kwanini usingewekeza sehemu ili
kuwe na mradi wa kuzalisha ndio
ununue gari?
6 .Una marafiki wengi ambao ni
mizigo kwako au hamuendani
kivipato hivyo unajikuta
unalazimika kutumia zaidi ya
kipato chako ili uwa-impress.
Meneja wa TRA na mwalimu wa
sekondari unatarajia utoe offer
mpaka umfurahishe Meneja?
Utabaki na sh ngapi toka kwenye
salary yako? Zinduka.
7. Huna timetable ya kudumu ya
maisha yako, unajikuta unaburuzwa
tu na marafiki zako kwa kwenda
sehemu mbalimbali za
matumizi.kuwa na ratiba za maisha
yako na zisimamie kikamilifu,
usiburuzwe!
8. Una michepuko inayokutegemea
wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM
wewe unakenua tu huzinduki.
Badilika.
9. Una huruma sana kuliko kipato
chako. Yaani kila ukiombwa unatoa
hata kama muombaji hana genuine
need. Usiwe mkristo kuliko Yesu.
Fanya hivyo kama ni lazima. Ila sio
kila anaekupiga mzinga unapigika.
10.Unatembea na hela nyingi
kwenye wallet au mshahara wote
kwenye wallet au handbag au
nyumbani kwako. Unapokuwa na
petty cash nyingi unatengeneza
mazingira ya kutumia hovyo.
Jifunze kuweka hela benki. Tembea
na hela tu unayoihitaji kwa
matumizi ya lazima.
Naamini tukizingatia kanuni hizi
kumi tutaongeza savings zetu na
kuwa na mtaji wa kufanya vitu
vikubwa endelevu
NB: MABADILIKO HUANZA NA
WEWE
No comments:
Post a Comment