Unatamani upate Mwenza wako,
yaani mke au mume, lakini unajiuliza mbona
kila uhusiano ukianza unaishia njiani na hujui
sa7bu
Nakwambia hiviii:
jichunguze kwanza.na Usikimbilie kwenda
kuombewa, kumtafuta mchawi kwa kusikiliza
maneno ya wapambe (hivi siku hizi wapambe
sio nuksi?) au kwenda kwa waganga ambao
watakulia pesa zako wakidai wana dawa ya
kurudisha mpenzi!
Kama una tabia ya kuomba omba ela wakati
ndio kwanza mahusiano yanaanza hapo
mwanamke lazima ile kwako , wanaume
hawapendi wanaomba omba ela ktk mwanzo
wa mahusiano, JICHUNGUZE
kama una tabia ya kila anapokupigia
mtarajiwa wako ukipokea simu cha kwanza ni
kuomba ela ya vocha alafu akikutumia wewe
ni kubeeb tu.JICHUNGUZE.
Kama una tabia ya ukali wa ajabu ajabu, kitu
kidogo tu ushatoa maneno kibao makali -
hujui maneno yanachoma kuliko upanga?
Tena hakuna yanayochoma zaidi kuliko
maneno makali toka kwa yule umpendaye.
Halafu ukiombwa msamaha ni mgumu kama
nini kusamehe. JICHUNGUZE
Kama ukikosea mwenzako akakwambia,
unakimbilia kununa na kukata mawasiliano,
utafikiri wewe haukosei. JICHUNGUZE.
Kama una wivu uliovuka mipaka. Ukimwona
mwenzio anaongea na mtu wa jinsia
nyingine, tena mahali pa wazi tu, unaanza
kuwa na mawazo ya ajabu ajabu na
kumwuliza maswali yasiyokuwa na kichwa
wala miguu.JICHUNGUZE
Kwani unadhani kabla hajakufahamu alikuwa
anaishi katika dunia ya watu wa jinsia yake
tu? Si nakuuliza wewe mwenye hii tabia?
JICHUNGUZE.
Kama kila mkiongozana kwenda shop au
kuwasiliana na mwenzako unachofanya ni
kutoa orodha ndeefu ya mahitaji, ambayo
yote yanahitaji pesa.Hata siku moja hujawahi
hata kum surprise kwa kumtumia hata ka elfu
mbili kwenye Mpesa, Tigopesa, Airtel money
na namba yake umeikariri kama sala huwezi
kusema huikumbuki! JICHUNGUZE
No comments:
Post a Comment