Nilikuwa naangalia mpira wa
miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa Nilimuuliza kijana
mmoja juu ya Matokeo ya
mchezo.
Kwa tabasamu, alijibu "Wako
mbele yetu 3-0"!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata
tamaa..?
Kukata tamaa?
Yule mvulana aliuliza kwa
mshangao…."!?
Kwanini nikate tamaa wakati
bado refa hajapuliza kipenga
cha mwisho?
Nina imani na timu yangu na
meneja wa timu; Nina hakika
tutashinda!
Na kwel mchezo uliisha 5-4
timu ya kijana ikiwa mbele!
Alinipungia mkono taratibu,
na tabasamu zuri akiondoka
uwanjani; nilishangaa,
mdomo wazi, ujasiri mkuu
kiasi hiki such beautiful
faith
Nilipofika nyumbani usiku
ule swali lake lilizidi kuja
kwangu zaidi
"Kwanini niogope wakati refa
hajapuliza kipenga cha
mwisho?"
»»»Maisha ni kama mchezo
Kwanini ukate tamaa wakati
mwenyezi Mungu ndiye
meneja wako?
Kwanini ukate tamaa wakati
kungalipo uhai ndani yako?
Kwanini ukate tamaa wakati
kipenga chako cha mwisho
bado hakijapigwa?
Ukweli ni kwamba watu
wengi hujipulizia wenyewe
vipenga vyao vya mwisho.
Lakini maadamu ungalipo
uhai, hakuna
kisichowezekana muda
haujakuacha.
Nusu kipindi si kipindi
kizima na ratiba ya Mungu
kwa mwanadamu si ratiba ya
mwanadamu kwa Mungu
Usijipulizie kipenga chako
cha mwisho we mwenyewe
JIPE MOYO USIKATE TAMAA!
KWA MUNGU YOTE
YANAWEZEKANA.
KAMWE USIKATE TAMAA.
No comments:
Post a Comment