Sisi wanafunzi wa enzi zile tulipokuwa shule
ya msingi tulifanya haya hebu vuta hisia
kidogo uwakumbuke wadau wako wa nguvu
wa enzi hizo
1.Unaenda shule umechelewa unakuta
mwalim anakamata wachelewaj unaamua
urudi nyumbani
2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua
sakafuni af unamuunguza mwenzio
3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa
kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4.MTU akikukera unamfungia shule
(mnapigana baada ya kufunga shule)
5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia
"Ahaa eeh utaona sa nne"
6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa
kusuta wenzao
7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata
uliloandika
8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass)
na mengine hayaandiki
9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata
kuvitumia mfano bikari labda utolee mwiba
10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo
hamna shule mwalim haupo
11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban
kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula
mgeni kaja tumempa
12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia
sweta begi na viatu vyake
13.usiombee umpige mtoto wa mwalim
utataman uache shule
14.unatengeneza kifutio cha ndala af
unatishia eti kinafuta hadi peni
15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba
chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji,
ukienda na naji wanakagua kuni au mbolea
Dah shule zetu hizi kiboko!!
Ipi umeipitia wewe
No comments:
Post a Comment