Tuesday, September 12, 2017

LEO YAKO

Leo ina thamani sana kuliko
kesho Jana imepita hatuwez
irudisha, kesho hatuna
utawala nayo, ila siku pekee
tuliyo na utawala nayo ni leo
Leo ndio muhimu
Unafanya
nini leo kwa ajili ya mipango
yako? Kitu unachofanya leo
ndio kinaonyesha kesho
utakuwa wapi Kama hakuna
unachofanya leo na
unategemea kufanya kesho
itakuwa ngumu sana kufikia
malengo na mipango yako
Kama una mpango wa
kuwekeza badae leo unafanya
nini kwa ajili ya huo mpango?
Kama una mpango wa
kuanzisha biashara leo
unafanya nini kwa ajili ya hiyo
biashara? Kama una mpango
wa kuwa mtu fulani ikifika
kipindi fulan leo unafanya
nini kuukamilisha mpango
wako

No comments:

Post a Comment