Monday, September 4, 2017

TUJIFUNZE KITU HAPA KUPITIA JARIBU HILI


Mkulima mmoja alikuwa na Punda ...Punda
aliyedumu nae kwa miaka mingi sana
aliyemsaidia shughuli za kilimo na
uchukuzi..alikaa naye toka akiwa mtoto
mpaka punda akawa mzee kabisa.
Siku moja wakiwa wanatoka shambani, kwa
bahati mbaya yule punda alitumbukia kwenye
kisima kirefu sana ambacho kwa wakati ule
kilikuwa kimekauka.
Yule Mkulima akawaza sana atafanyaje
kumtoa yule punda..na baada ya kutafakari
sana akasema kwanza hata hivyo huyu punda
ameshazeeka ni hasara kuingia gharama za
kumtoa...akaona vema tu amzike humo humo
Akaenda kuita majirani ,wakaja na sepetu
wakaanza kumwagia udongo ,mchaka na
kokoto shimoni kumfukia.
Mwanzoni tu ni kama punda alijua
kinachoendelea..akapaza sauti na kulia kwa
sauti kali ajabu..sauti ya malalamiko...ha
wakujali waliendelea kufukia..kwa kutupia kila
aina ya taka taka
Baadae kidogo kwa mshangao wa wengi
ghafla punda alinyamaza kimya kabisa sauti
ikapotea....baada ya kutupia taka
kadhaa..mkulima yule akaamua kuchungulia
shimoni....Alistushwa mno na alichokiona
Kila taka na mchanga ulipokuwa ukiangukia
mgongoni mwa punda...alikuwa akifanya kitu
cha kushangaza.
Kila udongo ulipomwangukia..alijitingisha
ukamwagika na akaukanyaga akainuka juu
kidogo...kila ulipokuja aliendelea kufanya
hivyo hivyo..hatimaye baada ya Muda
mkulima na majirani walishangaa kuona
amefika juu kabisa ya ukingo wa kisima na
akatoka kwa furaha kabisaa.
Kuna wakati maisha yanakurushia matakataka
ya kila aina,acha kulia na kupiga kelele,
jitingishe...yafanye ngazi..Kila jaribu
linalotupata ni ngazi ya kupandia.
Kamwe hatuwezi toka kwenye visima virefu
kwa kulia peke yake..bali kwa kupambana
kuchomoka.
Wacha waone uko kimya baada ya
makombora waliokurushia...yatake
yapange..yafanye ngazi ya kupandia...
Changamoto yeyote unayopitia sasa...ni
shimo na michanga..sisi ni zaidi ya
punda..acha kulia, jikung`ute, yakanyage
,nyanyuka juu, toka Kanyaga Twende

No comments:

Post a Comment