Wednesday, September 6, 2017

AFANYALO MUNGU HALINA MAKOSA

Mzee alikuwa akisafir huku mkono mmoja
alibeba jogoo na mwingine taa! katikati ya
safari yake giza lilianza kuingia hivyo
aliamua kuomba hifadhi kijiji cha jirani kwa
bahati mbaya hakuna aliye mkubalia mzee
akiwaza lakini akasema AFANYALO MUNGU
HALINA MAKOSA akaamua kwenda msituni
karibu na hicho kijij Akiwa amelala usiku ule
huku taa yake ikiwaka ghafla ulivuma upepo
mkali ukavunja taa kukawa giza kuu, mzee
aliinuka na kujisemea AFANYALO MUNGU
HALINA MAKOSA akaendelea kulala, Majira
ya saa nane usiku alishtuka na kukuta jogoo
wake hayupo vivyo hivyo akijisemea
AFANYALO MUNGU HALINA MAKOSA
Ilipofika asubuhi aliamka na kushangaa moshi
mkubwa katika kile kijiji Lo! kumbe kijiji
chote kimeteketea KUMBE angepokelewa
naye angeteketea Lo! KUMBE usiku ule
majambazi walipita karibu yake wangeona
mwanga wa taa wangeanza nayeye KUMBE
wale majambazi walitoka kijijin hapo saa
kumi angekuwepo yule jogoo angewika mida
hiyo wangejua huko kuna makazi na
kumteketeza,, AFANYALO MUNGU HALINA
MAKOSA!..mshukuru Mungu kwa kila jambo

No comments:

Post a Comment