Sunday, December 22, 2019

KACHA

KACHA

FAMILY

Hakuna Ambaye Atatoka Katika Haya Maisha Akiwa Na Uhai Wake, ifurahie Leo Na Omba Msaada Panapo Ulazima

MUDA

Kupuuzia Kitu Chochote Ambacho Hakina Msingi Katika Maisha Yako Ni Sehemu Ya Kutunza Muda Wako Vizuri

FIKRA

Kuwa Makini Na Unachofikiria Kila Siku, Fikra Zako Ndio Zinazoendesha Maisha Yako

TUKAE HUMO

Ni bora kunyamaza wakuambie ongea wewe , kuliko kuongea sana wakuambie kaa kimya wewe.

Tuesday, December 10, 2019

Tabia unazozifanya hadharani ni rahisi kuzibadilisha ama kuziacha kwakuwa zinaonwa hivyo zinapata wasemaji wengi. Ogopa sana tabia zako zile ambazo huzioneshi hadharani maana hizo mabadiliko yake yatatokana na wewe tu hakuna mwingine.

tambua

Ya dunia ni Mengi na huyawezi chagua, baadhi yatakayo kupa manufaa

SOMA HII

Kama huna nia ya kumsaidia mtu usitafute visingizio. Unaanza kumjaji mtu profile picha yake, anacho post, watu alio wafollow, muda anaotumia kuwa online, user name anayoitumia, unacho like na kucomment. Haya yote ya nini, yani awe mtumwa kwako kwa ahadi ya kumpatia mchongo

TUKAE HUMO

Kusema ni rahisi kuliko kufikiri.
Binadamu Wengi watatafuta kasoro zako kuliko hata uimara wako. Watambue halafu ishi nao

NI KWELI

Kama Ukitaka kupendwa na wengi, jiandae kuzungukwa na wanafiki wengi.

TUKAE HUMO

Usiwe mwepesi sana wa kukosoa kosoa, kisicho kufaa kitawafaa wengine.

TUKAE HUMO

Dharau si jambo jema, ila kuna vitu uki vidharau basi dharau hiyo hugeuka kuwa jambo jema. Kuna dharau positive na dharau negative.

TUKAE HUMO

Tumia hekima wakati unaongea, kumbuka wanao kusikiliza nao muda wao wa kuongea Utafika.

KIJIWEN

Ukipewa ushauri kijiweni kuhusu jambo fulani, jitahidi ulifanyie kazi fasta hilo jambo. Kijiweni sio nyumbani kwenu ambapo jambo moja linarudiwa rudiwa kila ukiamka. Wahuni hawanaga muda wa kurudia rudia ushauri, wakiutoa wamesha malizana na wewe

Dunia uwanja wa mashindano, watu hawata jali malalamiko yako, bali wanaangalia ushindi wao tu. Lalama huku ukitafuta solution.
Dunia uwanja wa mashindano, watu hawata jali malalamiko yako, bali wanaangalia ushindi wao tu. Lalama huku ukitafuta solution.
Punguza mipango, anza utekelezaji.
Acha watu waseme kile wanachokisikia ama wanacho tamani kukisikia kuhusu wewe. Kuwazuia wasiseme kuna muda unazuia darasa la bure la kujitambua.

JITAMBUE

Kwenye Maisha Kuna Vitu Flani Hivi Usipoamua Kuachana Navyo, Itakuchukua Muda Sana Kupata Maendeleo..
Furaha ya mtu inajengwa
na namna ambavyo MOYO WAKE UMERIDHIKA...
Ridhika ili uwe na AMANI na hicho unachoamini
hakina thamani maana wakati utakuja
UTAKITAFUTA USIKIPATE Kwani ndo uhalisia wa
nyakati, Ogopa kuishi kwa kuyafuata MACHO
Kwani utajikuta unakosa kujuwa CHENYE
THAMANI KWAKO.

JITAMBUE

Kuna wakati Macho yako
yanatamani kuona kile ambacho ubongo wako
unawaza lakini hata ukifumbua kwa nguvu kiasi
gani huwezi kuona hali hiyo tunaiita Upofu wa
Fikra, Katika kila mbio kila mmoja ana speed yake
katika kufikia kile ambacho anakikimbiza
haijalishi ni wangapi waliokikimbiza na kukipata
ila cha muhumu ni kuongeza Speed ili tu na wewe
ukipate, Maisha ni sawa na Muziki unaopigwa
Night Club na Dj Mzuri ila kila mmoja ana aina ya
uchezaji wake (Style) ila mwisho wa siku kila
mmoja anatengeneza Furaha yake. Usiige furaha
ya Mwenzako (Lifestyle) sababu haiwezi
kukufurahisha wewe kama vile inavyomfurahisha
yeye, Talanta huumba Brand Thabiti yenye kuruka
wenye kunakili na kukufuata wewe bila
kuilazimishia.

MAPENZI

Mapenzi hayalazimishwagi bali yanajengwa,
Fikiria zaidi AMANI kuliko hata FURAHA maana
usipoipa AMANI NAFSI YAKO kamwe hutokaa
uione FURAHA
Maana FURAHA NA AMANI ni pacha wasiofanana

MAISHA

katika maisha binadam tunapitia mengi sana adi
kufika pale unapostahili kuwa
kwenya maisha kuna changamoto nying sana
ambazo unatakiwa kuzikabili
na kweny maisha amin kwamba kila linalokuja
bas lilipangwa litokee usiwe mwepes wa kulaum
wala kulipa kisasi kwani huwez jua labda ulipo
sasahiv bila hichokisas unacholipa usingekua
hapo ulipo haijalish pazur au pabay lakin tambua
ndo njia ya kufika unapostahili kuwa.kikubwa na
cha msingi ni kuangalia kwa jicho la3 na kutafuta
njia ya kusolve na si kuandaa vita itakayo gharim
nafs yako kutokuwa na amani
Unajua upendo ni MATENDO YA NAFSI na kwa vyovyote vile ujumbe wa NAFSI huupa MOYO kuweka wazi NGUVU YA PENDO LILILOKO NDANI. Ni kweli tunashauliwa kuufuata MOYO

GM

Kulazimisha MAPENZI kwa Mtu ambaye hajui alikupenda lini na lini aliacha kukupenda ni Sawa na kuwasha MSHUMAA kwenye UPEPO Yaani kama hujakinga mikono yako UPEPO usiyumbishe uwakaji wa mshumaa lazima mshumaa utazima!

FAHAMU

Wakati unamlinganisha baba na Mama kudai Mama ni Bora kuliko baba shukuru baba kwa kukuchagulia Mama aliye bora

Upendo wa mama kwa mtoto hauzuiliki huja tu! lv u mom

KUNA MABINTI  ALAFU KUNA SALIMA
Sometimes tuna-fake smile ili kuficha makovu mioyoni mwetu. Sio kila anayetabasamu ana furaha moyoni.