Sunday, December 22, 2019

KACHA

KACHA

FAMILY

Hakuna Ambaye Atatoka Katika Haya Maisha Akiwa Na Uhai Wake, ifurahie Leo Na Omba Msaada Panapo Ulazima

MUDA

Kupuuzia Kitu Chochote Ambacho Hakina Msingi Katika Maisha Yako Ni Sehemu Ya Kutunza Muda Wako Vizuri

FIKRA

Kuwa Makini Na Unachofikiria Kila Siku, Fikra Zako Ndio Zinazoendesha Maisha Yako

TUKAE HUMO

Ni bora kunyamaza wakuambie ongea wewe , kuliko kuongea sana wakuambie kaa kimya wewe.

Tuesday, December 10, 2019

Tabia unazozifanya hadharani ni rahisi kuzibadilisha ama kuziacha kwakuwa zinaonwa hivyo zinapata wasemaji wengi. Ogopa sana tabia zako zile ambazo huzioneshi hadharani maana hizo mabadiliko yake yatatokana na wewe tu hakuna mwingine.

tambua

Ya dunia ni Mengi na huyawezi chagua, baadhi yatakayo kupa manufaa

SOMA HII

Kama huna nia ya kumsaidia mtu usitafute visingizio. Unaanza kumjaji mtu profile picha yake, anacho post, watu alio wafollow, muda anaotumia kuwa online, user name anayoitumia, unacho like na kucomment. Haya yote ya nini, yani awe mtumwa kwako kwa ahadi ya kumpatia mchongo

TUKAE HUMO

Kusema ni rahisi kuliko kufikiri.
Binadamu Wengi watatafuta kasoro zako kuliko hata uimara wako. Watambue halafu ishi nao

NI KWELI

Kama Ukitaka kupendwa na wengi, jiandae kuzungukwa na wanafiki wengi.

TUKAE HUMO

Usiwe mwepesi sana wa kukosoa kosoa, kisicho kufaa kitawafaa wengine.

TUKAE HUMO

Dharau si jambo jema, ila kuna vitu uki vidharau basi dharau hiyo hugeuka kuwa jambo jema. Kuna dharau positive na dharau negative.